Jul 16, 2008

Ajali tena ziwa Victori

Mbali na ajali mbaya iliyotekea miaka ya 1996 katika ziwa Victoria ambayo haitasahaulika ajali zingine zimezidi kulikumba Ziwa hilo ambapo watoto 11 waumini wa madhehebu ya sabato (SDA) wakiwemo wanane wa shule ya msingi Kitangaza,Wilaya ya ukerewe wamekufa maji katika Ziwa Victoria,wakisafiri kwenda kwenye mahubiri. Ajali hiyo ilitokea Jumapili iliyopita saa 10.00 katika kijiji cha Msonga wakati waumini 30 wa SDA wakisafiri kwa mtumbwi wa injini kwenda kijiji cha Kamenya .watu wote waliokuwemo walizama ambapo ndugu hao na waumini wengine wakubwa waliokoka kwa kuogelea,watoto11 wakafa maji

No comments: