Eneo la Mwanagati lipo Ilala kwenye mradi wa viwanja 20,000 vilivyopimwa na Wizara ya Ardhi maendeleo ya makazi mwaka 2004.
Katika upimaji huu yalitengwa maeneo ya makazi,shule,viwanja vya michezo,ofisi za serikari,masoko,sehemu za ibada nk.Lakini Mwanagati hii kwa siku za hivi karibuni imekuwa tishio kwa uvamizi wa majambazi tena mapema ya saa 1 usiku.
Yapo matukio mengi yametokea lakini mimi nimeshuhudia mawili, mwishoni mwa January2010 jirani yangu nyumba kama ya3 kutoka kwangu alivamiwa saa2 usiku bahati nzuri yeye na mkewe walikuwa hawaja rejea toka kazini,katika tukio hilo risasi zililindima kutuogofya ,mlinzi alipigwa nondo na kumvunja mguu wa kushoto ila alifanikiwa kuruka ukuta na kujiokoa,majambazi yalifanikiwa kupora la3 unusu.
Tukio la pili limetokea jana jion mida ileile kwa mzee Clement Kuzwa ,ni mita chache kutoka kwenye hiyo picha hapo juu, wamepora,wamemjeruhi,haya majambazi yameigeuza mwanagati kuwa sehemu ya tishio kwa watu na malizao.
Ombi langu kwa serikali itujengee kituo cha Polisi kwani tunategemea ya Kitunda ambacho kipo mbali na sisi. Hata tukitoa taalifa maaskari maranyingi wanafika baada muda na majambazi yanakuwa yameshatoweka.
No comments:
Post a Comment