May 12, 2008

ZE COMEDY WABWAGA MANYANGA !!!

Kundi mahiri la vichekesho la Ze Comedy' ambalo lilikuwa likirusha vichekesho hivyo kupitia kipindi cha 'Ze Comedy' Show' kwenye kituo cha Televisheni cha Channel 5 (EATV), kiraejiengua kutoka kwenye tv hiyo.
Akitangaza uamuzi huo siku ya Ijumaa kwenye ukutnbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mkurugenzi wa 'Ze Comedy' Production, Isaya Mwakilasa maarufu kama Wakuvanga', alisema kuwa walikuwa na mkataba na EATV na baada ya kuifanya kazi hiyo kwa miezi minane mkataba umekwisha hivyo wameamua kumpumzika kwa muda mpaka hapo baadaye.
Mkurugenzi huyo mwenye sauti ya kitoto, akiwa ameambatana na akina Joti, alisema, wameamua kupumzika ili wawe huru huku wakianza kuangalia wafanye kazi na nani badala ya EATV.
"Tumeamua kupumzika sisi kama sisi, imani yetu ni kuamua kupumzika kwanza. Maana tumekuwa tukifanya kazi na EATV hadi kufikia hapa," alisema Wakuvanga.
Hata hivyo, kiongozi huyo alishindwa kuutaja muda gaini watakuwa mapumzikoni au watafanya kazi na nani
Akasema kundi hilo lililoondokea kuwa gumzo nchini, kwa sasa wamelisajili na kujulikana kwa jina la Ze Comedy Production lenye makazi yake jijini Dar es Salaam.
Naye aliyekuwa meneja wa kundi hilo ambaye pia ndiye mbunifu mkubwa, Sekione David ' Seki' au 'John mvaa Viatu, amedai hajui kwa sasa afanye nini kwani yuko katika wakati mgumu kati ya kuamua kupumzika na wenzake hao au kuendelea na kazi EATV.
Alisema ni uamuzi wa kijasiri Sana kwani siku za nyuma alishawahi kupata wakati mgumu kama huo.
Kwa upande wake Wakuvanga aJisema kuwa, vipindi vyote vya Ze Comedy vitivyokuwa vikirushwa na EATV rii mali ya kituo hicho.
Hata hivyo, habari nyingine zilidai kuwa, wasanii hao wenye kurudia matukio yaliyopita, wanatarajiwa
kujiunga na Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TBC) kama wasanii wa vichekesho.
Wakuvanga alipoulizwa kuhusu tetesi hizo, hakutaka kuweka wazi kwa kukubali au kukataa na hivyo kuwafanya wenye akili zao waanze kuamini ukweli fulani.
Siku ya Alhamisi, kituo cha Telvisheni cha Channel 5 kilirudia vipindi vya Ze Comedy vya zamani huku watazamaji wake wengi wakiamitii kuwa, ni mpangilio wa kuboresha zaidi kwa kutoa kumbu kumbu za 'iamani.
Inaseniekana uongozi wa EATV ulilazimika kurudia vipindi vya nyuma ili kwenda na mikataba ya matangazo walivokuwa wanayapata kutoka kwa makarnpuni mbalimbali kwa lengo la kutumia kipindi hicho.

Kundi hilo linaundwa na

Isaya Mwakilasa (mkurugenzi), Emmanycl Mgaya 'Maasanja' (mkurugenzi msaidizi), Alex Chalamila ' Mac Reagan' ambaye pia ni Afiaa wa mipango, Mujuni Silvery Mpoki' ambaye ni afisa wa Masoko, Lucas Mhuville 'Joti' na Joseph Shamba ' Vengu'.

1 comment:

Anonymous said...

Good words.