Oct 8, 2007

AOA MKE ANAYE MZIDI MIAKA 34

Bonny mika 24 akiwa na Mke wake Nakacwa mika 58

Mchunga amewa fungisha ndoa Bonny Kayondo miaka 24 na mke wake Margaret Nakacwa miaka 58,aliwatakia kwenda kuishi na amani pamoja na kuzaa watoto kuongeza dunia.Ndoa hii imefungwa huko Uganda baada ya Bonny Kayondo na Margaret Nakacwa kukubaliana kwenda kanisani na kufunda ndoa hadharani.
Minongono kadhaa ilisikika kwa baadhi ya waumini wakisema 'Kayondo umefuata nini kwamke huyo ambaye ni kama Mama yako kabisa? ''huyu mama kamuua uzazi mtoto wa watu''
Kayono anasema hivi alionana na Nakacwa Mwezi wa 11 mwaka 2006.''Nilichompendea mke huyu sio hela ila tabia zake nzuri na nnaimani kwamba tutazaa watoto'' Hivyo ndivyo alivyo lijulisha jarida moja maarufu huko Nchini Uganda mara baada ya kufunga ndoa na mke wake.

Naye Mke anasema kwamba ,kilichompelekea afunge ndoa na Kayondo ni Mapenzi aliyo muonesha tangia wawe pamoja pia amemsahaulisha mateso analiyopata kutoka kwa Mme wake wa kwanza.Hata hivyo Nakacwa alika taa kutaja sababu ya msingi zilizosababisha kuvunjika kwa ndoa yake ya kwanza

No comments: