Tufikiri soko letu la ndani vijana wa Kitanzania
Karibuni wapendwa wasomaji katika makala hii kwa wakati mwingine tena mkiwa nami mwanaharakati wenu na kama kawaida huwa napenda kutoa changamoto kwa vijana wenzangu na leo ningependa tukae na tufikiri kuhusu soko letu la ndani sisi vijana wa kitanzania ambao ndio hasa Taifa la leo.
Tunavionaje vikapu, makatambuga,nguo za vitenge,batiki, bazee na bidhaa nyingine kibao ambazo kwa ujumla vinatengenezwa kwa sana hapa hapa nyumbani na watengenezaji wake wengi ni watanzania wenyewe na hii ni hasa kwa sababu ni vitu kama vya utamaduni wetu sema tu vimewekwa kisasa ili tu kuendana na mabadiliko ya kimazingira kwa sasa kwa mfano ukiona kikapu ambacho kinauzwa sasa ni kama pochi inayotengenezwa kiwandani tena viwanda vyenyewe vile vya nchi za mbali ambao tunatambua kwamba wenzetu hawa wametutangulia kiteknolojia kidogo.Lakini
pamoja na hayo unanunua kikapu kile ndugu? Na katika kuonyesha kwamba sisi vijana kweli hatujitambui kama wewe ni mtu wa kutembea tembea hapa na pale kwa siku moja tu unaweza kukutana na watu hasa vijana hata wanaozidi kumi tena watanashati wakiwa wamevaa nguo hasa fulana eti
I LOVE ---------eti nchi au mji wa Ulaya au Amerika nini maana yake sasa inakusaidia nini wewe unalipwa? na hata ungekuwa unalipwa yaani ndio uuze utaifa wako? Huo ndio utumwa wa kiakili sasa.
Kama kawaida niliongea na vijana kadhaa na kwa bahati nzuri walikuwa ni wanafunzi wa sekondari wa ngazi ya juu
(A-level) na nilitumai kwamba tutazungumza vizuri kidogo kwa sababu wamepiga hatua kidogo kielimu au kwa upande mwingine naweza kusema sio sawa na wale waliopo nyumbani tu au walioishia darasa la saba.Twende mbele turudi nyuma mdahalo ulikuwa mgumu kidogo maana nilianza na mambo ambayo yanaendana na
vijana nilianza kwa kuwauliza kama ni wapenzi wa muziki wa nyumbani na wote waliniambia wanapenda na nilihoji ni muziki wa aina gani na wote walisema ni mashabiki wazuri wa “Bongo flavour” na hakukuwa na neno na hapo hapo niliwakandamiza swali jingine kwamba mara ngapi wananunua albamu za wasanii mbalimbali wa “Bongo flavour”? hapo sasa watu wakaanza kujiuma uma ooh!sijui nini sikutaka kuendelea na hilo nikawauliza tena kama wanapenda miziki ya mabara mengine ukiachana na Afrika na jibu lilikuwa ndio nikauliza kama huwa wananunua albamu za huko na kwa kujiamini kabisa walisema ndio tena bila aibu nilishangazwa na jibu hilo tena kutoka kwa wanafunzi kama wale na hapo kama kawaida yangu nikaanza kushusha somo la nguvu kwa nini wasianze kujifanya wanaongea kwa kiingereza na kifaransa! ujinga ule ule wanarudia na mimi nae kwa lugha hizo kidogo sijambo basi wee si miraha hiyo.
Tukiachana na hayo yaliyonikuta katika harakati zangu ambayo ilinibidi niwashirikishe nirudi kwako
wewe, je?kama unaipenda nchi yako haswa na unajithamini kwa nini basi huvai nguo iliyoandikwa TANZANIA au kwa nini basi unashabikia bidhaa za GUCCI sana na kujisifu juu wakati huna ya URAFIKI au KTM hata moja au ndio umaarufu basi leo nakwambia ni ujanja kati ya wajinga. Sikatai mtu kuvaa nguo au bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na makampuni ya nje lakini nategemea nguo zinazotengenezwa kwenu ziwe nyingi zaidi, matokeo yake ukitembelewa na mgeni anayetokea nchi za nje nikimaanisha nje ya Afrika,
Unakuta yeye ana nguo za kwenu nyingi kuliko wewe kwanza wewe mwenyewe unaona aibu basi tu unajikaza na kujifanya unaenda na wakati.
Ukimuona kijana ananunua nguo zinazosifu sifu nchi yake au ananunua nguo za kiasili hapo ujue anaenda nje ya nchi sasa ya kazi gani ili wakuone? Sasa inakusaidia nini?
Kama usipojitambua mwenyewe nani atakutambua?
Maoni niandikie:
Email:neemafivawo@yahoo.com
No comments:
Post a Comment