Jul 10, 2007

JE WATOTO NI TAIFA LA KESHO

Kuna usemi maarufu sana wa kiswahili usemao ‘Watoto nii Taifa la kesho’.Maranyingi usemi huu hutamkwa kwa madaha na watu wazima wakijaribu kuonyesha jinsi gani wanawapenda watoto na vijana na jinsi watoto na vijana hao walivyo muhimu kwa taifa.

Lakini hebu ngoja kwanza tutafakari.Kama sisi ni taifa la kesho, na leo je? Iwapo utawasikiliza kwa makini watuwazima wengi,utabaini kuwa usemi wao huo una maanisha kwamba bado sisi tupo kwenye maadalizi..Nikama kwamba sisi si watu kamilibali ni malighafi zinazotaka kuchongwa kuwa watu wazima au watu kamili.Wakati mwingine usemi huu unaleta hizia kuwa hivi sasa sisi hatuna thamani na umuhimu wowote hadi pale tu tutakapokuwa watu wazima.

Iwapo sisi ni muhimu hivi leo, basi basi watu wazima wanahitaji kutuchukulia maanani.Maoni yetu hayasikilizwi.Hisia zetu zina puuzwamawazo yetu yana tupiliwa mbali ,Aidha, hatushirikishwi kufanya maamuzi yawe madogo au hata makubwa.

Ukweli nikuwa watoto na vijana tuna maoni mengi ya kutoa na mengi ya kuchangia kuhusu maisha yetu na maisha ya jamii yetu kwa ujumla .Tua hisia mawazo,mashaka na mipango yetu ambayo inaweza kabisa kuwa na manufaa kwa jamii.Yote yanahitaji kusikilizwa.

Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa haki za Mtoto ni sheria ya kimattaifa inayo tambua na kubainisha kuwa watoto na vijana walio chini ya miaka 18 ni Binadamu kamili na muhimu kama walivyo watu wengine.Viwili kati ya mkataba huu ninasema.
“Wakati wote jamii inapofanya maamuzi mbalimbali, ni budi mambo yanayo wagusa au kuwaathiri watoto na vijana yapewe kipaombele” (kifungu cha 3). Kwa mfano, hii inamaanisha kuwa, serikari ihakikishe kuwa sekta ya elimu,afya na hata viwanja vya kuchezea watoto vinapatiwa fedha za kutosha kabla hizo fedha hazijatumika katika mambo mengine, mathalani, matumizi ya kijeshi au ununu zi wa magari ya kifahari kwa viongozi.

Maoni ya Watoto pia ni muhimu.Hivyo basi, wapatiwe fursa ya kushiriki katika kufanya maamuzi yanayogusa mambo yao (kifungu 12).Hii inamaanisha kuwa ni vyema watoto na vijana wasikilizwe si wanapo kuwa nyumbani bali pia shuleni na katika jamii kwa ujumla.Aidha, ni budi washirikishwe kikamilifu katika kufanya maamuzi kuhusu mambo mbali mbali ikiwa pamioja na maisha ya kifamilia, jinsi ya kuendesha shule zao na hata kuhusu utendaji wa serikali.

Hii hii haimaanisha kuwa watoto wana haki ya kujifanyia maazi yoyote wao wenyewe, bali ina maanisha kuwa watoto ni watu wazima wanaweza kushirikiana , kuheshimiana na kusikiliza kwa makini mawazo na maoni ya kila upande ili kupata maoni mazuri zaidi na hatimaye kufikia maamuzi mazuri yatayo jail maslahi na haki za kila upande..Tunaweza kujifunza kutoka kwa watu wazima ambao mara nyingi wana uzoefu, busara na hekima nyingi,Lakini pia watu wazima wanaweza kujifunza mengi kutokana na busara na mawazo ya watoto na vijana.
Karubu nchi zote Duiani ikiwemo Tanzania ,Zimetia saini kuadhimisha mkataba huu wa wa Haki za Mtoto .Hivyo basi ,nchi hizo zinawajibika kuufata na kuutekeleza kwa vitendo mkataba huu na hivyo kuufanya hai miongoni mwa jamii katika nchi hizo.

Tunahitaji sana msaada wako ili kuifanya Dinia yetu iwe mahali bora zaidi kwa watoto na vijina.Mchango wako japo wa sauti unaweza kuleta mabadiliko! Hisia,maoni na mawazo yako yanahitajika sana .Soma gazeti hili n a lichangie na wenza.Kisha jadilianeni ni jinsi gani mtaweza kuboresha maisha yenu wenyewe, ya familia zenu n ya jamii kwa ujumla
Ishi kama Taifa la leo!

Mosesi Mbakile

No comments: