Serikali imebadilisha picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete kufuatia ushauri wa wataalam kwamba picha ya sasa haifai kuendelea kutumika kwa kuwa inaonyesha dalili uchovu wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.Picha inayotumika sasa ilipigwa mara tume ya uchaguzi kumtangaza Kikwete kuwa mshindi wa urais wa mwaka 2005.Kulingana na umuhimu wa picha ya Rais katika katika idara mbalimbali ikiwemo idara ya Mahakama,ndiyo maana picha hiyo ililazimika kutumika wakati huo.Nakala ya picha mpya ya rais yenye vipimo vipya itauzwa Tsh 15,000 na zitapatikana mapema mwezi ujao.
Jun 27, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment